Maelezo
Haya ni mafunzo yanayohusiana na utengenezaji wa mikate, keki, maandazi, biscuits, pastries pamoja na vyakula vingine vya bakery. Kozi hii huwasaidia wanafunzi kupata ujuzi wa kitaalamu wa kupika na kupamba bidhaa za bakery kwa ubora unaovutia wateja. Mafunzo haya yanafaa kwa wanaotaka kujiajiri au kufanya kazi kwenye hotel, bakery na migahawa.
Mafunzo yanatolewa darasani na kwa njia ya mtandao
Vitu Tunavyojifunza Ndani ya Kozi Hii
- Utengenezaji wa mikate ya aina mbalimbali.
- Kutengeneza keki na mapambo yake.
- Utengenezaji wa pastries kama donuts, pies na cookies.
- Matumizi sahihi ya oven na vifaa vya bakery.
- Namna ya kuchanganya viungo kwa vipimo sahihi.
- Uhifadhi wa bidhaa za bakery na usafi wa mazingira ya kazi.
- Mbinu za biashara na kuwahudumia wateja.
Faida za Kujifunza Kozi Hii
- Unaweza kuanzisha bakery yako mwenyewe na kupata chanzo kizuri cha kipato.
- Kuongeza ubunifu katika mapishi na mapambo ya vyakula.
- Unaweza kutengeneza bidhaa kwa matumizi ya nyumbani na biashara.
