Maelezo
Haya ni mafunzo ya awali ya ushonaji kwa vitendo na nadharia yanayotolewa kwa muda wa miezi mitatu. Mafunzo haya huwasaidia wanafunzi kupata ujuzi wa kushona nguo mbalimbali kwa ubora na ubunifu.
Ushonaji ni moja ya taaluma muhimu inayoweza kumsaidia mtu kujiajiri au kupata ajira kwenye sekta ya mavazi na mitindo.
Vitu utakavyojifunza kwenye masomo ya ushonaji
- Jinsi ya kutumia mashine ya kushonea.
- Kupima na kukata vitambaa kwa usahihi.
- Kushona nguo za wanawake, wanaume na watoto.
- Kutengeneza patroni (patterns).
- Ubunifu wa mitindo ya kisasa ya mavazi.
- Namna ya kufanya marekebisho ya nguo.
- Utunzaji wa mashine za ushonaji.
- Mbinu za biashara ya ushonaji na huduma kwa wateja
Kwa nini tujifunze ushonaji
- Kupata ajira au kujiajiri kwa urahisi.
- Kuongeza kipato kupitia biashara ya nguo.
- Kuwa mbunifu katika sekta ya mitindo.
- Kusaidia jamii kupata mavazi bora na yenye ubora.
- Kujenga uwezo wa kujitegemea kiuchumi.
- Kupanua fursa za kazi mbalimbali kwenye ushonaji
