Ufungaji wa mifumo ya kusambaza na kutibu maji

Sambaza:


Maelezo

Tunabuni, kufunga na kusimamia mifumo ya usambazaji wa maji kutoka kwenye visima hadi kwenye maeneo ya matumizi. Huduma zetu zinajumuisha uwekaji wa mabomba, mifumo ya kusukuma maji na miundombinu mingine muhimu inayowezesha maji kufika kwa ufanisi katika makazi, taasisi, viwanda na migodi.

Pia tunatoa huduma za ufungaji wa mifumo ya Reverse Osmosis (RO) kwa ajili ya kutibu maji na kuboresha ubora wake. Teknolojia hii husaidia kuondoa chumvi, madini yasiyotakiwa na uchafu mwingine unaoweza kuathiri usalama na ubora wa maji ya matumizi ya binadamu.

Kwa kuunganisha mifumo ya usambazaji na utibuji wa maji, tunawasaidia wateja kupata maji salama, safi na yanayofaa kwa matumizi mbalimbali. Kila mradi hubuniwa kulingana na mahitaji halisi ya mteja na mazingira ya eneo husika.

Hakuna!
Bidhaa
Tafuta
Huduma