Maelezo
Tunatoa huduma za ushauri wa kitaalamu kwa miradi ya Tailings Storage Facilities (TSF), kuhakikisha miradi ya migodi inatekelezwa kwa kuzingatia mahitaji ya kiufundi, kimazingira na kisheria. Huduma hizi ni muhimu kwa migodi inayohitaji kujenga au kuboresha maeneo ya kuhifadhi mabaki ya uchakataji wa madini.
Huduma zetu zinajumuisha maandalizi ya nyaraka na tafiti mbalimbali zinazohitajika katika hatua za upangaji na uidhinishaji wa TSF. Hii ni pamoja na TSF design, hydrogeological reports, hydrological reports, topographical surveys, geotechnical reports pamoja na environmental reports.
Kwa uzoefu wetu katika nyanja za maji, mazingira na uhandisi, tunasaidia wateja kuandaa nyaraka zinazokidhi matakwa ya wadau na mamlaka husika. Lengo letu ni kuhakikisha miradi ya TSF inajengwa kwa usalama, ufanisi na kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
