Maelezo
Biashara au taasisi haiwezi kukua kwa mafanikio bila kuwa na mfumo mzuri wa uendeshaji. Strategy Bridge Point tunasaidia biashara, kampuni, NGOs na taasisi mbalimbali kujenga mifumo na miundo inayowezesha ukuaji wa muda mrefu.
Tunatoa huduma zinazohusisha usajili wa taasisi, maandalizi ya Company Profiles, uundaji wa Organizational Structures na ushauri wa kiutawala unaosaidia kuongeza ufanisi wa kazi ndani ya taasisi.
Lengo letu ni kuhakikisha taasisi yako haifanyi kazi kwa mazoea pekee, bali inakuwa na mifumo inayotambulika, inayoaminika na inayorahisisha ukuaji.
Company Profiles
Company Profile ni kitambulisho rasmi cha biashara au taasisi yako. Hii ndiyo nyaraka inayomweleza mteja, mdau au mwekezaji wewe ni nani, unafanya nini na kwa nini anapaswa kufanya kazi na wewe.
Tunakuandalia profile yenye muonekano wa kitaalamu, maudhui yenye nguvu na mpangilio unaoonyesha historia, huduma, mafanikio na dira ya taasisi yako.
Company Profile bora huongeza uaminifu wa biashara yako na kukupa nafasi nzuri katika zabuni, mikataba na fursa mbalimbali za kibiashara.
NGOs, Trusts na Company Registration
Kuanzisha taasisi au kampuni kunahitaji kufuata taratibu za kisheria na kiutawala. Tunakusaidia katika mchakato mzima wa usajili wa NGOs, Trusts, Companies na aina nyingine za taasisi.
Tunatoa mwongozo wa hatua kwa hatua kuanzia maandalizi ya nyaraka, kujaza fomu husika mpaka kufanikisha usajili kwa mamlaka zinazohusika.
Kwa uzoefu wetu, tunarahisisha mchakato ambao mara nyingi huonekana mgumu na unaochukua muda mrefu kwa watu wengi.
Organizational Structures
Kadri taasisi inavyokua, ndivyo umuhimu wa kuwa na mfumo mzuri wa majukumu na mamlaka unavyoongezeka. Tunakusaidia kuandaa Organizational Structure inayobainisha idara, nafasi za kazi na mfumo wa uwajibikaji.
Muundo huu husaidia kupunguza migongano ya majukumu, kuongeza uwazi na kuboresha mawasiliano ndani ya taasisi.
Matokeo yake ni taasisi inayofanya kazi kwa ufanisi zaidi, yenye mfumo unaoeleweka na unaowezesha ukuaji endelevu.
