Maelezo
Watu wengi wana mawazo mazuri ya biashara lakini hawajui waanzie wapi. Wengine wana biashara tayari lakini wanakosa mwelekeo wa ukuaji. Kupitia huduma yetu ya Business Consultation, tunakuwa mshauri wako katika safari nzima ya biashara.
Tunatoa ushauri wa kitaalamu unaokusaidia kufanya maamuzi sahihi kuanzia hatua ya wazo, uanzishaji wa biashara, kujenga chapa (Brand) mpaka uendeshaji wa kila siku.
Huduma hii imeundwa kwa ajili ya wafanyabiashara wanaotaka kupunguza makosa, kuongeza faida na kujenga biashara inayoweza kukua kwa muda mrefu.
Wazo la Biashara
Kila biashara kubwa huanza na wazo. Tunakusaidia kuchambua wazo lako ili kujua kama lina soko, linaweza kuleta faida na lina nafasi ya kukua.
Tunafanya tathmini ya fursa zilizopo sokoni, ushindani na mahitaji ya wateja ili kuhakikisha unaanza biashara yenye msingi mzuri.
Badala ya kuanza kwa kubahatisha, unapata mwongozo unaokusaidia kufanya maamuzi sahihi tangu mwanzo.
Brand Identity (Logo, Colors, Business Cards n.k.)
Brand si logo pekee. Brand ni namna watu wanavyoitambua na kuikumbuka biashara yako. Tunakusaidia kujenga utambulisho wa biashara unaoendana na malengo yako na soko unalolenga.
Huduma hii inajumuisha ushauri wa logo, business cards, company colors, brand guidelines na vitu vingine vinavyojenga taswira ya biashara yako mbele ya wateja.
Brand yenye nguvu huongeza uaminifu, hujenga tofauti dhidi ya washindani na huifanya biashara yako ionekane ya kitaalamu zaidi.
Usajili na Uendeshaji wa Biashara
Baada ya kupata wazo na kujenga brand, hatua inayofuata ni kuendesha biashara kwa mfumo sahihi. Tunakushauri kuhusu usajili, leseni, taratibu za kisheria na mifumo ya msingi ya biashara.
Pia tunakupa mwongozo wa namna ya kusimamia shughuli za kila siku, kupanga malengo ya biashara, kuwahudumia wateja na kuandaa mikakati ya ukuaji.
Lengo ni kuhakikisha biashara yako haianzi tu, bali inakuwa na uwezo wa kuendelea kukua, kushindana sokoni na kuzalisha matokeo ya kudumu.
