Maelezo
Nikon D5100 ni kamera yenye uwezo mkubwa wa kupiga picha zenye ubora wa juu inayokuja na lenzi ya 18-55mm na image sensor ya megapikseli 16.2. Ni nzuri kwa matumizi binafsi au kikazi kwenye kurekodi na kupiga picha za harusi, matukio, na mandhari mbalimbali.
VIPENGELE MUHIMU
- Aina ya Kamera: DSLR (Digital Single-Lens Reflex)
- Image sensor: CMOS ya megapikseli 16.2, kinachotoa picha zenye uwazi na rangi halisi.
- Lenzi: Inakuja na lenzi ya 18-55mm VR (Vibration Reduction) inayosaidia kupunguza mtikisiko wa kamera wakati wa kupiga picha.
- Kioo cha Kuangalia (LCD): Kioo cha inchi 3 chenye Vari-Angle, kinachozunguka kwa urahisi kwa ajili ya kupiga picha kutoka pembe mbalimbali.
- Video: Ina uwezo wa kurekodi video za Full HD (1080p) kwa ubora wa hali ya juu.
- ISO: Inasapoti kiwango cha ISO kutoka 100 hadi 6400, kinachowezesha kupiga picha katika mwanga hafifu bila kupoteza ubora.
- Modi za Kupiga Picha: Ina modi mbalimbali za ubunifu kama vile HDR, Night Portrait, na Close-up kwa picha za karibu.
- Muundo: Imetengenezwa kwa muundo mwepesi lakini imara, rahisi kubeba na kutumia.





