Afilieti ni jukwaa la mtandaoni linalowaleta pamoja wauzaji na wanunuzi kwa urahisi zaidi. Kupitia jukwaa hili, wauzaji wanaweza kupakia bidhaa zao kwenye akaunti zao huku wateja wakipata nafasi ya kuona bidhaa hizo na kuwasiliana moja kwa moja na wauzaji.
Tunachokiamini
Tunaamini kila mfanyabiashara anastahili nafasi ya kuweka biashara yake mtandaoni bila kulazimika kuwa na tovuti binafsi. Ndiyo maana tumeunda mazingira rahisi na yenye lugha ya Kiswahili ili kusaidia biashara zetu kukua kidijitali.
Dira yetu Afilieti
Dira yetu ni kuwa kituo kinachoaminika cha biashara mtandaoni kinachowaunganisha wajasiriamali na wateja wao moja kwa moja. Lengo letu ni kukuza upatikanaji wa bidhaa, kuongeza mwonekano wa biashara ndogo, na kurahisisha manunuzi kwa kutumia teknolojia ya mtandao.

Karibu Afilieti
Sehemu rahisi ya kuonyesha, kugundua, na kununua bidhaa mtandaoni!
Wasiliana nasi kwa maulizo, maoni, mapendekezo au lolote kuhusu Afilieti kupitia
admin@afilieti.store