A3/A4 Heavy-Duty Laminator

Maelezo

A3/A4 Heavy-Duty Laminator ni mashine bora ya kulamineti iliyoundwa kwa ajili ya matumizi ya ofisi, shule, maduka ya huduma, na biashara nyinginezo. Ikiwa na uwezo wa kulamineti hadi ukubwa wa karatasi wa A3, mashine hii ni chaguo bora kwa kazi ndogo na kubwa.

VIPENGELE MUHIMU

  • Uwezo Mpana wa Kulamineti: Inakubali karatasi za ukubwa wa kratasi ndogo zaidi na ukubwa wa hadi A3, ikikupa uhuru wa kushughulikia nyaraka za ukubwa tofauti.
  • Teknolojia ya Roller Nne: Imeundwa na roller 4 zenye nguvu zinazohakikisha usambazaji wa joto sawia na kulaminati laini bila mikunjo au mabaki ya hewa.
  • Usalama wa Hali ya Juu: Imetengenezwa kwa viwango vya usalama vya kisasa, mashine hii ni salama kutumia hata kwa watumiaji wapya – hakuna hatari ya kuunguza au kuharibu nyaraka zako.
  • Udhibiti wa joto: Unaweza kushusha na kuongeza (adjustable) nyuzi joto hadi ~ 180°C. Pia ina mfumo wa “hot” na “cold” lamination – unaweza kuchagua lamination ya joto (thermal) au ya baridi.
  • Kurudisha nyuma (Reverse function): Hii inapunguza hatari ya kujeruhi nyaraka ikiwa kuna jam.
  • Rangi ya Kisasa: Inapatikana katika rangi ya kijivu (grey) inayofaa mazingira yoyote ya kazi au biashara.

FAIDA ZA A3/A4 Heavy-Duty Laminator

  • Uwezo mpana: Inalamineti nyaraka ndogo (ID cards, picha) hadi kubwa (A3 posters).
  • Ulinzi wa nyaraka: Hufanya karatasi kuwa sugu kwa maji, vumbi, na kuchanika.
  • Matokeo ya kitaalamu: Uso laini, glossy au matte kulingana na pouch.
  • Ufanisi wa muda: Inalamineti haraka na kwa wingi bila kuharibika.
  • Urahisi wa kutumia: Wengi wana paneli rahisi ya kudhibiti joto na kasi.

MATUMIZI YANAYOPENDEKEZWA

  • Ofisi: Kulinda nyaraka muhimu (vyeti, mikataba, leseni).
  • Shule: Kulamineti mitihani, flashcards, na mafunzo ya darasani.
  • Biashara: Menus, posters, price lists, na signage.
  • Nyumbani: Picha za familia, vyeti vya watoto, au kumbukumbu.

TAHADHARI za matumizi ya A3/A4 Heavy-Duty Laminator

  • Tumia pouches sahihi (80–250 microns) kulingana na mashine.
  • Usilamineti karatasi yenye moto au unyevu.
  • Hakikisha mashine imepata joto sahihi kabla ya kuanza.
  • Fanya usafi wa rollers mara kwa mara ili kuepuka mabaki ya adhesive.

MAELEKEZO KWA VIDEO

Emma, Kilangi, Makoroboi - Stendi ya daladala, Mwanza, -, Tanzania
Hakuna!
Bidhaa
Aina
Tafuta
Akaunti