Maelezo
Airtel 5G Router ni kifaa chenye teknolojia ya kisasa kutoka Airtel kinachokupa kasi ya intaneti ya 5G kwa urahisi popote ulipo. Kinafaa kwa matumizi ya ofisini au kazini, na familia nyumbani.
Zipo Indoor Unit (IDU) ambazo zinakaa ndani na Outdoor Unit (ODU) ambazo zinakuja nakifaa cha kufunga nje ili kuongeza uwezo wa kunasa mawimbi ya mtandao na Wi-Fi kufika mbali zaidi
Unaweza kusogeza router mahali popote ili kupata ishara nzuri ya 5G.
VIPENGELE MUHIMU
Mtandao wa 5G: Inakupa intaneti ya kasi mpaka 5G na kusambaza WiFi mpaka mita 100.
Kuunga vifaa vingi: IDU ina uwezo wa kuunga vifaa mpaka 32, na ODU vifaa mpaka 64 sambamba na WiFi,kwa wakati mmoja.
Rahisi kutumia: Plug-and-play – unachukua router, unaunganisha, na kuanza ku-share WiFi kwa simu, tablet, laptop bila kuwa na mbinu ngumu.
Sambamba na 4G/3G: Kama 5G haikupatikana, router hii pia hukupa uwezo wa kutumia 4G na 3G, hivyo haina tatizo kwenye maeneo yenye mtandao mdogo.
Mipangilio: Unaweza ku-manage router yako kupitia simu yako kama vile kuseti jina la Wi-Fi, kubadili nenosiri, kuruhusu au kutoruhusu matumizi kwa watu (vifaa vingine) nakadhalika.
GHARAMA NA VIFURUSHI
Kwa mara ya kwanza utafungiwa pamoja na kulipiwa kifurushi cha mwezi mzima (unlimited internet) kwa 100,000/=
Vifurushi vyake ni matumizi bila kikomo kwa mwezi;
70,000/Mwezi – 25Mbps
100,000/Mwezi – 40Mbps
Chapakazi Bundles – Members benefit 10GB, Dakika 1000 & SMS/Mwezi
150,000/Mwezi – 20Mbps – 3 members
200,000/Mwezi – 30Mbps – 5 members
300,000/Mwezi – 30Mbps – 9 members
400,000/Mwezi – 50Mbps – 15 members





