Maelezo
Caesar K ni mbolea ya majani yenye ubora wa hali ya juu yenye Potassium (K20) 11% na Silicon (SiO2) 22%, virutubisho vinayoongeza uimara wa mmea na kuusaidia kustahimili hali ngumu kama ukame na mashambulizi ya magonjwa
Mbolea hii:
- Husaidia kuimarisha mizizi na kuongeza ukuaji wa majani yenye afya
- Hufyonzwa haraka na mimea kwa matokeo yanayoonekana mapema
- Huongeza maua, ukubwa wa matunda na ubora wa mazao
- Husaidia mimea kuvumilia ukame, magonjwa na mazingira magumu
- Inafaa kwa mahindi, nyanya, mboga za majani, mpunga, matunda na mazao mbalimbali ya biashara
Kwa kutumia Caesar K, mkulima hupata mimea yenye nguvu, mazao yanayovutia sokoni na mavuno yenye kuongeza kipato. Ni mbolea rahisi kutumia lakini yenye matokeo makubwa kwa kilimo cha kisasa.
