Maelezo
1: Utambulisho
Casio fx-991ES Plus ni kalkuleta ya kisasa ya kisayansi inayotumika kwa masomo ya hesabu, fizikia, kemia, uhandisi na takwimu. Ina uwezo wa kufanya mahesabu mengi kwa haraka na kwa usahihi mkubwa. Kalkuleta hii ina mfumo wa “Natural Display” unaoonyesha mahesabu kama yalivyo kwenye kitabu.
2: Sifa za Bidhaa
- Ina zaidi ya 417 functions za kihesabu.
- Mfumo wa Natural Textbook Display kwa uandishi rahisi wa formula.
- Ina uwezo wa kufanya hesabu za: Algebra, Trigonometry, Statistics, Fractions, Integration na Differentiation Complex Numbers
- Skrini kubwa inayosomeka kwa urahisi.
- Muundo mdogo na mwepesi kubeba.
- Betri hudumu kwa muda mrefu.
- Inafaa kwa wanafunzi wa sekondari, vyuo na wataalamu.
3: Matumizi Makuu
- Kutatua maswali ya hesabu za kawaida na za kisayansi.
- Kufanya mahesabu ya asilimia, mizizi na logarithms.
- Kutumika kwenye masomo ya: Mathematics, Physics, Chemistry, Engineering, Statistics
- Kusaidia wanafunzi wakati wa mitihani na mazoezi ya darasani.
- Kufanya uchambuzi wa takwimu na grafu za kihesabu.
4: Maelekezo ya Matumizi
- Bonyeza kitufe cha ON kuwasha kalkuleta.
- Chagua aina ya hesabu unayotaka kupitia kitufe cha MODE.
- Andika hesabu yako kwa kutumia vitufe husika.
- Bonyeza kitufe cha = kupata majibu.
- Tumia kitufe cha SHIFT kupata functions za ziada.
- Zima kalkuleta baada ya matumizi kwa kubonyeza SHIFT + AC (OFF).
- Epuka kuangusha au kulowanisha kifaa ili kudumisha ubora wake.
