Chain Saw 24″ – Heavy Duty

Sh 850,000

Maelezo

Chain saw ni kifaa cha kisasa cha kukatia miti au mbao, kinachotumia minyororo yenye meno makali inayozunguka kwa kasi juu ya blade (bar). Tofauti na msumeno wa kawaida unaotegemea nguvu ya mkono, chain saw hutumia injini ya petroli, umeme au betri kukamilisha kazi kwa haraka, kwa ufanisi, na kwa nguvu kubwa.

 

HUSQVARNA 272XP – 24″ Bar Chain Saw

Hii ni chain saw ya kiwango cha kitaalamu kutoka kampuni maarufu ya Husqvarna, yenye Urefu wa blade: Inchi 24 (takriban sentimita 60) na Nguvu ya injini zaidi ya 70cc, inayotumia petroli na inakuwa na Tool Box yake.

 

VIPENGELE MUHIMU

  • Nguvu na kasi kubwa: inakata kwa haraka na kwa ufanisi hata kwenye miti mikubwa au mbao ngumu, hivyo hukamilisha kazi kwa muda mfupi.
  • Matumizi madogo ya mafuta: Injini yake ina ufanisi mkubwa wa mafuta, hivyo hupunguza gharama za uendeshaji kwa muda mrefu.
  • Uhakika wa kudumu: Ina blade ndefu na imara, vipuri vinapatikana kwa urahisi, na muundo wake ni wa kuaminika kwa matumizi ya muda mrefu.
  • Muundo wa Heavy Duty: Imetengenezwa mahsusi kwa kazi nzito na mazingira magumu.Inafaa kwa kazi zifuatazo:
    • Kukata miti mikubwa na minene
    • Kufyeka mashamba yenye vichaka vikubwa
    • Kukata mbao na kuni kwa matumizi ya ujenzi au biashara
    • Kazi za bustani, mashamba na misitu

 

MAELEKEZO KWA VIDEO

Joack, Company, Tegeta - Wazo hill, Dar es Salaam, -6.667650,39.173965, Tanzania
Hakuna!
Bidhaa
Aina
Tafuta
Akaunti