Flash Drive (4 in 1)

Sh 25,000

Maelezo

Flash Drive (4 in 1) ni kifaa kidogo kinachofanana na flashdisk ya kawaida, lakini tofauti yake kubwa ni kwamba ina konekta (vichomeo) vinne tofauti — unaweza kuitumia kwa simu, tablet, au kompyuta bila kutumia nyaya (cable).

Flash hii 1 inakuwa na sehemu 4 za kuunganisha (ports):

  1. USB Type-A – kwa kompyuta au laptop za kawaida
  2. USB Type-C – kwa simu/laptop mpya zenye chaji kama za Android au baadhi ya MacBook
  3. Micro USB – kwa simu za zamani zinazotumia chaji ndogo (kama zile za kabla ya Type-C)
  4. iPhone Lightning – kwa baadhi ya modeli maalum za OTG flash zinazoendana na simu za iPhone

Kwa hiyo, unaweza kuhifadhi na kuhamisha picha, video, muziki au mafaili kati ya simu na kompyuta bila kutumia cable ya data.

 

VIPENGELE MUHIMU

Uwezo: Inapatikana kwa ukubwa tofauti kama 32GB, 64GB, 128GB au 256GB

Kasi: Ikiwa ni ya USB 3.0 au 3.1, inaweza kusoma hadi 100MB/s na kuandika hadi 30–50MB/s

Mfumo: Inafanya kazi na Android, Windows, Mac OS, iPhone (kwa baadhi ya modeli)

Muundo: Imetengenezwa kwa aluminium alloy na plastiki imara, na mara nyingi ina keyring ya kubebea

 

FAIDA ZAKE

  • Rahisi kutumia – unachomeka tu, inafanya kazi (Plug & Play)
  • Unaokoa nafasi ya simu – hifadhi picha na video zako kwenye flash badala ya simu
  • Uhamisho wa haraka – kutoka kwa simu kwenda PC au kinyume chake
  • Inafaa kusafirisha kazi au data muhimu bila kutumia mtandao
  • Inaendana na vifaa vingi – hauhitaji flash tofauti kwa kila kifaa

 

UKUBWA – BEI

  • 32GB – 25,000/=
  • 64GB – 35,000/=
  • 128GB – 40,000/=

MAELEKEZO KWA VIDEO

Mzigo, Express, Korogwe, Dar es Salaam, -, Tanzania
Hakuna!
Bidhaa
Aina
Tafuta
Akaunti