Maelezo
Garmin GPSMAP H1 ni kifaa cha GPS cha kisasa kinachotumika kuonyesha location na kuhifadhi njia ukiwa field, porini au maeneo ya kazi ngumu. Kina usahihi mkubwa hata sehemu zenye milima, misitu au network mbaya.
Kina screen ya touch pamoja na button za kawaida hivyo ni rahisi kutumia hata ukiwa na glavu, mvua au matope. Betri yake inadumu muda mrefu sana na kina ramani tayari ndani pamoja na uwezo wa kuweka memory card.
Kifaa hiki ni kigumu na kinastahimili maji, vumbi na mapigo, hivyo kinafaa kwa safari za porini, wachimbaji wa madini, survey, utafiti, wakulima, maafisa field na watu wanaopenda adventure.
Pia kina tochi yenye mwanga mkali na king’ora cha dharura kwa usalama zaidi.
