Maelezo
HUSQVARNA 272XP-24″Bar ChainSaw ni msumeno wa kisasa wa kukatia miti au mbao kutoka kampuni maarufu ya Husqvarna, yenye Urefu wa blade: Inchi 24 (takriban sentimita 60) na Nguvu ya injini zaidi ya 70cc, inayotumia petroli na inakuwa na Tool Box yake.
VIPENGELE MUHIMU
- Uwezo wa silinda: 72.2 cm³
- Nguvu ya injini: 3.6 kW (takribani 4.8 hp)
- Kasi ya mnyororo kwa nguvu ya juu: 20.7 m/s
- Urefu wa bar: 24 inch (takribani 60 cm)
- Aina ya mnyororo: H42
- Crankshaft: Imetengenezwa kwa vipande vitatu vilivyoforgiwa kwa uimara wa juu
- Crankcase: Magnesium, imara na sugu kwa rpm kubwa na matumizi ya muda mrefu
- Oil Pump: Adjustable – unaweza kurekebisha kiwango cha mafuta kulingana na mahitaji ya kazi
- Anti-vibration system: Inapunguza mtetemo ili kulinda mikono na kupunguza uchovu
- Smart Start®: Teknolojia inayorahisisha kuwasha injini kwa haraka na bila tabu
Faida za HUSQVARNA 272XP-24″Bar ChainSaw
- Nguvu na kasi kubwa: inakata kwa haraka na kwa ufanisi hata kwenye miti mikubwa au mbao ngumu, hivyo hukamilisha kazi kwa muda mfupi.
- Matumizi madogo ya mafuta: Injini yake ina ufanisi mkubwa wa mafuta, hivyo hupunguza gharama za uendeshaji kwa muda mrefu.
- Uhakika wa kudumu: Ina blade ndefu na imara, vipuri vinapatikana kwa urahisi, na muundo wake ni wa kuaminika kwa matumizi ya muda mrefu.
- Muundo wa Heavy Duty: Imetengenezwa mahsusi kwa kazi nzito na mazingira magumu.Inafaa kwa kazi zifuatazo:
-
- Kukata miti mikubwa na minene
- Kufyeka mashamba yenye vichaka vikubwa
- Kukata mbao na kuni kwa matumizi ya ujenzi au biashara
- Kazi za bustani, mashamba na misitu
Tahadhari na matunzo ya HUSQVARNA 272XP-24″Bar ChainSaw
- Hakikisha unatumia mafuta sahihi ya injini na mnyororo ili kuongeza maisha ya mashine.
- Kagua mara kwa mara bar na chain kwa ajili ya mikato safi na usalama.
- Tumia PPE (Personal Protective Equipment) kama gloves, helmet, na chaps wakati wa kutumia.
- Fanya service ya mara kwa mara ili kudumisha utendaji bora.
MAELEKEZO KWA VIDEO




