Hydrogeological & Hydrological Surveys

Sambaza:


Maelezo

Tunafanya tafiti za hydrogeology na hydrology kwa ajili ya kukusanya na kuchambua taarifa muhimu kuhusu maji chini ya ardhi na maji ya juu ya ardhi. Tafiti hizi husaidia kuelewa mwenendo wa maji katika eneo husika na kutoa msingi wa maamuzi sahihi katika miradi mbalimbali.

Katika huduma za hydrogeological surveys, tunachunguza uwepo, mwelekeo na tabia ya maji chini ya ardhi kwa ajili ya miradi ya uchimbaji wa visima, ujenzi wa miundombinu na shughuli za migodi. Kwa upande wa hydrological surveys, tunachambua mifumo ya maji ya juu ya ardhi, ikiwemo drainage patterns na athari zinazoweza kutokea kutokana na mtiririko wa maji.

Matokeo ya tafiti hizi hutumika katika upangaji wa miradi, tathmini za mazingira, usimamizi wa rasilimali za maji na maandalizi ya nyaraka za kiufundi. Tunatoa taarifa na mapendekezo yanayosaidia wateja kufanya maamuzi yenye tija na yanayozingatia mazingira.

Hakuna!
Bidhaa
Tafuta
Huduma