Maelezo
Kitabu cha Kanuni 20 za Fedha ni mwongozo wa elimu ya kifedha unaolenga kukufundisha namna ya kutengeneza, kutunza na kuwekeza fedha kwa usahihi.
Kitabu hiki kinatoa misingi ya utunzaji na uwekezaji wa fedha, kikiwa na kanuni 20 zinazokusaidia kujenga nidhamu ya kifedha na kuondokana na matumizi yasiyo na mpangilio.
Baadhi ya mambo utakayojifunza ni
- Vichochea vya Mafanikio ya Kifedha (Tabia zinazoleta Utajiri)
- Dhana potofu kuhusu utajiri na mafanikio ya kifedha
- Jinsi ya kutengeneza Bajeti na kuishi kwa Bajeti
- Jinsi ya kujenga nidhamu ya kuweka akiba
- Elimu ya Uwekezaji kwenye Hisa, Hatifungani na UTT Amis.
Popote ulipo Tanzania unaweza kukipata na kwa wakazi wa Dar tunaweza kukuletea ulipo.


