Maelezo
Portable power station (150W) ni kifaa chenye nishati ya umeme kinachobebeka, suluhisho bora kwa mahitaji ya umeme wa haraka na wa kuaminika, hasa katika mazingira yenye changamoto za umeme au maeneo yasiyo na umeme.
Kina mfumo unaokupa umeme wenye uwezo wa kuendesha vifaa mbalimbali ikiwemo TV, friji, feni, kompyuta, kuchaji simu na vifaa vingine popote ulipo. Pia kina taa ya LED inayotoa mwangaza mkubwa wa hadi 200 lumen, bora kwa matumizi ya nje au dharura.
Vipengele muhimu vya Portable power system (150W)
- Nguvu ya 150W: Inatosha kuendesha vifaa vidogo kama simu, laptop, taa, feni ndogo, na vifaa vya elektroniki vya nyumbani.
- Betri ya ndani (Rechargeable): Ina betri inayoweza kuchajiwa tena kwa kutumia soketi ya kawaida, solar panel, au gari.
- Porti nyingi za kuchaji: USB, DC, na AC outlets kwa matumizi tofauti.
- Muundo compact na mwepesi: Rahisi kubeba na kutumia popote.
- Ulinzi wa usalama: Ina mfumo wa kuzuia overload, short-circuit, na overheating.
- AC output voltage: 110V/220V
- AC rated output power: 150W
- DC output: 12V
- DC input: 12.6V/5A
- Battery capacity: 12.8V40AH
Faida kwa Mtumiaji wa Portable power station (150W)
- Uhuru wa nishati: Huna haja ya kutegemea umeme wa gridi kila wakati.
- Inafaa kwa safari na shambani: Bora kwa camping, safari ndefu, au maeneo yenye upungufu wa umeme.
- Urahisi wa matumizi: Plug-and-play, haina ugumu wa kiufundi.
- Thamani ya pesa: Inaokoa gharama za mafuta ukilinganisha na jenereta ndogo.





