Maelezo
SITUKA M1 ni aina ya mbegu ya kisasa ya mahindi (Zea mays L.) ambayo ni imara dhidi ya magonjwa, yenye mavuno mazuri iliyosajiliwa rasmi mwaka 2001 AR-Selian, kituo cha utafiti wa kilimo kilichopo Arusha, chini ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).
Ni moja kati ya mbegu bora kutoka kampuni ya Rieta Agrociences zilizoandaliwa kwa ajili ya mazingira ya kitanzania. Mbegu hii inawahi kukomaa na inastawi maeneo yenye mvua chache.
SITUKA M1 inapatikana kwa ujazo wa kilo 2.
SIFA KUU ZA MBEGU YA SITUKA M1
- Urefu wa mmea: takribani sentimita 180–195
- Muda wa kuchanua (50% flowering): siku 70–75
- Muda wa kutoa nywele (50% silking): siku 78
- Aina ya punje: mchanganyiko wa flint/dent (punje ngumu na laini)
- Rangi ya tassel: zambarau (purple)
- Mavuno: wastani wa tani 3.0–5.0 kwa hekta
Ustahimilivu na Kinga
- Ina uvumilivu dhidi ya maize streak virus na grey leaf spot.
- Ina usugu dhidi ya magonjwa kama:
- Diplodia
- Fusarium
- Leaf blight
- Puccinia sorghi (ugonjwa wa kutu)
Maeneo Yanayofaa kwa Kilimo
- Altitude: 1000–1500 m juu ya usawa wa bahari
- Inafaa zaidi kwa mikoa ya Morogoro, Arusha, Manyara, Singida na mikoa mingine yenye mvua chache
Umuhimu kwa Mkakati wa Kilimo
- SITUKA M1 ni mbegu ya Open Pollinated Variety (OPV), ikimaanisha mkulima anaweza kutumia mbegu zake kwa misimu 2–3 bila kupoteza sana ubora.
- Inafaa kwa wakulima wadogo wanaohitaji mbegu zenye gharama nafuu, mavuno ya uhakika, na kinga dhidi ya magonjwa ya kawaida ya mahindi.
- Kwa Tanzania, hii mbegu imekuwa sehemu ya jitihada za kuondokana na mbegu za kienyeji zenye mavuno madogo na zisizo na kinga thabiti.
Mwongozo wa kilimo cha mahindi





