SuperGro – Mbolea Asilia

Sh 60,000

Maelezo

SuperGro ni kirutubisho bora cha mimea kisicho na kemikali kilichotengenezwa kutokana na mimea, kinyesi cha ndege na wanyama. Ni mbolea ya kimiminika inayochanganywa na maji, inatumika kwenye mazao ya aina zote ikiwemo maharage, mahindi, kunde, viazi, korosho, chai, kahawa, kabichi, ngogwe, vitunguu, Karoti  na mazao mengineyo kwa kupandia, kukuzia, na kuzalishia.

Mbolea hii ya asili inatengenezwa na kampuni kubwa duniani ya NEOLIFE tangu mwaka 1958 na imeidhinishwa na wakulima duniani kote kwa uwezo wake wa kuongeza mavuno na ubora wa mazao bila kuharibu udongo. Imefanyiwa utafiti na vyuo vikuu vya kilimo duniani ikiwemo Chuo cha SUA Tanzania na imesajiliwa kihalali kwa matumizi ya kilimo.

 

VIRUTUBISHO MUHIMU – 1L

Nitrogen (N) 7.5%, Phosphorus (P) 4.5%, Potassium (K) 3.3, Zink (Zn) 0.1% na Calcium (Ca) 0.8%

 

KAZI KUU TATU ZA SUPERGRO

  1. Hulainisha maji na kuondoa mzio wa maji. Kama water surfactant mbolea hii oevu husaidia ukuaji wa mimea kwa kufanya maji kupenya hadi tabaka la tatu la udongo ambalo huwa na madini na virutubisho vingi muhimu kwa mimea. Kwa Kawaida maji mengi hutiririka juu ya udongo na majani ya mimea bila kupenya ardhini na kiasi kidogo tu hupenya na kuishia tabaka la juu la udongo, Jua likiwaka maji hayo hupotea kama mvuke hewani.
  2. Huwezesha mizizi kupenya na kufika mbali zaidi ili kwenda kujichukulia rutuba ambayo haijafikiwa kabisa na sumu yoyote hivyo mmea kuweza kuwa bora sana.
  3. Huchochea ufanyaji kazi mzuri wa mbolea na viwatilifu kuweza kufanya kazi vizuri pia hunatisha dawa zisiondolewe na mvua au hewa kirahisi, hivyo kupunguza gharama.

 

FAIDA ZA MATUMIZI YA SUPERGRO

  1. Kutunza unyevu kwenye ardhi
  2. Inasaidia mizizi ya mimea kupenya hadi kwenye tabaka la tatu la udongo kuchukua virutubisho
  3. Inafanya mimea ikue haraka na kwa usawa
  4. Inafanya mimea iwe na rangi ya kijani halisi
  5. Inakinga magonjwa ya ukungu au fangasi
  6. Inarudisha rutuba asilia iliyopotea kutokana na mbolea za chumvichumvi.
  7. Inafanya maua yasipukutike
  8. Inaongeza ukubwa na uzito wa mazao
  9. Inasaidia dawa nyingine zisitoke mapema kwenye majani.
  10. Inaongeza mavuno maradufu (utavuna mara 2–3 zaidi ya kawaida).
  11. Inapunguza gharama za pembejeo, kwani mbolea hii pekee inatosha.

 

BEI NA UJAZO

  • Lita 1: Tsh 60,000 – inatosha kwa ekari 2
  • Lita 5 (Offer maalum): Tsh 170,000 – inatosha kwa ekari 5

 

JINSI YA KUTUMIA

  • Changanya 1ml ya mbolea kwa kila lita 1 ya maji. Mfano: kama pampu yako ina ujazo wa lita 16, changanya na mbolea 16mls; kwa lita 20, changanya na 20mls.
  • Inafaa kwa misimu yote ya kilimo: Kwenye kiangazi tumia kila baada ya siku 7, kwenye masika tumia kila baada ya siku 14.

 

KWA MAHARAGE NA SOYA

  • Kabla ya kupanda loweka mbegu kwa masaa manne kwenye mchanganyiko wa SuperGro na maji. wakati wa kupanda acha nafasi ya sentimita 30 au rula moja kila moja kila upande kati ya mbegu na mbegu.
  • Badaa ya kuota puliza maharage yakiwa na majani mawili au matatu.
  • Wakati wa mvua pulizia mara moja kila baada ya wiki mbili na mara moja kwa wiki wakati wa kiangazi (ukame) puliza awamu mbili tu kisha upishe zoezi la upevukaji.
  • Ukiona maua yemeanza kutoka na wadudu waharibifu wapo changanya 15mls ya duducyper kwenye super gro mililita 15 na maji lita 15, kisha puliza kila baada ya wiki mbili au moja mpaka maua yatakapokomaa na kudondoka yenyewe. Baadhi ya sehemu huko Uganda wameweza kuvuna chini ya miezi miwili baada ya kupanda.
  • Kwa baadhi ya maneo yaliyofanyiwa utafiti mbegu ya kilo 5 iliweza kutoa mpaka kilo 250 ya mavuno.

 

KWA MAHINDI NA MTAMA

  • Loweka mahindi kwenye mchanganyiko wa 1ml ya Super Gro na lita 1 ya maji kwa masaa 12 kisha yaopoe.
  • Panda kati ya futi moja na nusu na futi mbili, mbegu mbili kila shimo.
  • Kama shamba lililozoea mbolea inashauriwa upandie na mbolea kidogo ila kadri unavoweka superGro rutuba inarudi kuwa kawaida.
  • Puliza baada ya mahindi kuota majani mawili hadi manne au urefu wa nusu futi. Endelea kupulizia mara moja kila baada ya wiki mbili wakati wa mvua na mara moja kwa wiki kama kuna ukame pulizia kwenye majani na ardhi kuzunguka shina. Kiangazi ni awamu 5 masika ni awamu 3.
  • Usipulize wakati mahindi yamefunga mimba ya mbelewele ili kupisha zoezi la upevushaji. Ila mazao yakibeba tu ruksa kuendelea kupuliza mpaka mahindi yatakapo toa hindi au mbele wele.
  • Inashauriwa kuchanganya na dawa za kuua wadudu kama kuna wadudu.
  • Unapotumia superGro Mahindi yana uwezo wa kutoa hindi mapema baada ya wiki 6 na yatakuwa tayari kuvunwa yakiwa mabichi baada ya miezi mitatu.
  • Matokeo ya kutumia Super Gro huko Masaka Uganda kilo 5 za mahindi yaliyopandwa zilitoa mavuno ya takribani kilo 6,000

 

KWA KARANGA

  • Kwa zao la karanga mbegu inashauriwa kulowekwa kwa saa 4 tu, Panda mistari kati ya nusu futi kila upande na mbegu moja kila shimo. Puliza mchanganyiko wa superGro na maji (1ml superGro kwa lita 1 ya maji)
  • Baada tu ya kuota puliza mara moja kila baada ya wiki moja wakati wa ukame na mara moja baada ya wiki mbili wakati wa mvua.
  • Acha kupulizia mara zinapoacha kutoa maua.

 

KWA VIAZI VITAMU

  • Loweka vipande vya miche sehemu ambazo zitazikwa ardhini ndio iingie kwenye mchanganyiko wa SuperGro na maji kwa saa 12 .
  • Baada ya kupanda na ukaona kama mizizi imeshika basi pulizia juu na endelea kupulizia mara moja kila wiki wakati wa ukame na mara moja baada ya wiki mbili wakati wa mvua hadi awamu 3.
  • Acha kupuliza baada ya majani kutambaaa na kufika tuta la pili yake.
  • Watumiaji wazoefu wa super gro wanasema baada ya wiki mbili hadi tatu viazi vichanga hufika ukubwa wa kidole
  • SuperGro hulainisha udongo na kuhifadhi maji kwenye matuta wakati wa kiangazi na viazi vinaweza kuendelea kuzaa hata mwaka mzima.

 

KWA VIAZI MVIRINGO (ULAYA)

  • Pulizia SuperGro kwenye mbegu usiku na kesho yake panda. Baada ya kuota pulizia kila baada ya wiki mbili mpaka vitakapoanza kutoa maua

 

KWA KAHAWA

  • Kwa mimea kama miti pulizia na mwagilia kuzunguka shina.
  • Weka nusu lita ya mchanganyiko wa SuperGro na maji kwenye mmea mmoja, ila ukiwa mkubwa utaweka lita au lita 2.
  • Huu mmea unatakiwa kupuliza kila baada ya wiki 2 msimu wa masika na wakati wa kiangazi usipulize.
  • Wakati kahawa inatoa maua pulizia superGro bila kuweka dawa yeyote ya kuua wadudu.
  • Matokeo ya mbuni mmoja huweza kutoa hadi kilo 20kg za kahawa iliyokobolewa.

 

KWA MIGOMBA/NDIZI

  • Kabla ya kupanda loweka shina la mgomba kwa saa 24 baada ya kupanda weka superGro kwa kufuata utaratibu kama ulotumia kwenye kahawa pia unaweza tumia kwenye dawa ya kuua magugu.

 

KWA MBOGA ZA MAJANI NA VIUNGO

  • Loweka mbegu kwenye mchanganyiko wa SuperGro na maji kwa siku mbili kabla ya kupanda, unaweza kupanda kwenye vitalu au moja kwa moja kwenye shimo.
  • Kwa kuwa mbegu huwa zinashikana ni vizuri kuziachanisha kabala ya kupanda.
  • Mbegu huota baada ya siku 5 tu ukilinganisha na kawaida ambapo huota baada ya siku 14 kwa nyanya.
  • Pia mchanganyiko huo wa maji na superGro utamsaidia mkulima kuondokana na adha ya kumwagilia mara kwa mara. angalau kila baada ya siku tatu badala ya kila siku na kuongeza uwezo wa mimea kufyonza Mbolea na virutubisho vingine kutoka Ardhini.

 

⚠️ANGALIZO

  1. Usizidishe kiwango, ukizidisha mmea haufi ila utadumaa na kuwa njano.
  2. Ukigundua umeharibu, kachanganye kwa usahihi upulize tena, kichwa kitaoza ila muhindi au zao lako litatoa matawi kama ya kupamba upya.
  3. Kwa kuwa SuperGro haiui wadudu, changanya na dawa ya kuua wadudu waharibifu kwa mazao ambayo hujichavua yenyewe.
  4. Mazao ambayo huchavuliwa na wadudu inashauriwa usitumie madawa ya kuua wadudu wakati mazao hayo yakitoa maua kwani dawa hizo zinaweza kuua wadudu wanaofanya uchavushaji.

 

SHUHUDA ZA WATUMIAJI KWENYE VIDEO

Mkoka, Shop, -, Dar es Salaam, -, Tanzania
Hakuna!
Bidhaa
Aina
Tafuta
Akaunti