Tepu ya kufukuza ndege

Sambaza:

Biashara:  Seeda Equipments

Maelezo

Linda mazao yako dhidi ya uharibifu unaosababishwa na ndege kwa kutumia hii Bird Tape Repellent. Tepu hii maalum hutumia mng’ao mkali unaoakisi mwanga pamoja na kelele inayotokana na upepo kuwafukuza ndege bila kutumia kemikali au kuwaua. Ni njia salama, rahisi na yenye ufanisi ya kulinda mazao yako.

Inafaa kwa mpunga, mtama, ulezi, wele, mahindi, bustani za matunda, na mazao mengine yanayoshambuliwa na ndege

Sifa za Bidhaa:

  • Hufukuza ndege kwa mng’ao na sauti zinazosababishwa na upepo.
  • Haina kemikali, hivyo ni salama kwa mazao, watu na mazingira.
  • Rahisi kufunga na kutumia shambani.
  • Inastahimili matumizi ya nje kwenye mazingira ya kawaida.
  • Husaidia kupunguza upotevu wa mazao na kuongeza mavuno.

Linda mazao yako kwa njia rahisi na yenye gharama nafuu ukitumia Bird Tape Repellent.

Hakuna!
Bidhaa
Tafuta
Huduma