Ukombozi wa fikra

Sambaza:

Sh 50,000

Biashara:  Global publishers

Maelezo

Mara baada ya kupata Uhuru wa Bendera, Mwl. Julius Nyerere alielekeza nguvu katika Uhuru wa Fikra maana aliamini bila Ukombozi wa Fikra, watanzania wataendelea kuishi utumwani. Kwahiyo akapeleka vijana wengi karibu kila kona ya dunia kuutafuta Ukombozi wa Fikra kupitia elimu. Lakini kwa bahati mbaya wengi wakaenda kupambana na mitihani badala ya ujinga. Wakarudi na fikra hatarishi kwa rasilimali za nchi. Mpaka mwalimu anaondoka duniani watanzania bado tunamwayamwaya katika Uhuru wa Bendera.

Mwalimu katuachia uhuru ambao mwenye nacho ndio binadamu na asiyenacho ni takataka. Uhuru wa wachache kuishi kama malaika na wengi kuishi kama mashetani. Uhuru unaowagawa watu kwa kipato na elimu. Uhuru wa bendera ni sawa na kuvaa suruali isiyo na zipu harusini. Uhuru wa bendera umetujengea nidhamu ya woga kwa manufaa ya wachache kutunyonya kutokana na uoga wetu. Tunahitaji uhuru kamili. Ule uhuru unaoanzia kichwani, yaani uhuru wa fikra. Uhuru utakaotusaidia kuyaona mambo katika uhalisia wake. Kichwani pakiwa vizuri hatutapoteza muda kukimbizana na samaki bwawani kama tunataka kuwakamata. Badala yake ni kuwakaushia maji yote tu.

Kumbuka “Fikra zinazoongoza akili yako ni muhimu zaidi ya kiasi cha akili ulizo nazo,” alisema David J. Schwartz kupitia kitabu chake cha, “The Magic of Thinking Big.” Fikra sahihi zinahitaji utulivu wa akili. Kuwa na muda wa kufikiri ndilo chimbuko la maendeleo yote duniani. Tunahitaji kuwa na karakana za kufikiri akilini. Badala ya kufikiri umaskini tulionao ni mapenzi ya Mungu, tufikiri umaskini kama matokeo ya kutofikiri vizuri.

Mungu ametupa rasilimali nyingi ambazo kama zingelitumika kwa faida yetu, zingeliweza kutuinua tukawa matajiri. Tufikiri kwanza ndipo tutende. Kwame Nkrumah alisema, “Matendo pasipo mawazo ni upofu, mawazo pasipo vitendo ni utupu.” Kumbe saa ya ukombozi wa fikra ni sasa. Tusitegemee kama kuna mtu atakuja kutukomboa isipokuwa ni sisi wenyewe aliimba Bob Marley katika kibao cha, “Redemption.”

Bila fikra huru tutaendelea kushuhudia watawala wakishindana katika matanuzi. Akinunua BMW, mwenzake ananunua Benz. Hii ndio itikadi ya Bongo. Kumbuka, “Leo upo pale ambapo mawazo yako yamekuleta, kesho utakuwa pale ambapo mawazo yako yatakupeleka. Mtu anavyofikiria katika akili yake anakuwa hivyo, na anavyochagua anakuwa hivyo.” Kumbe tuna kila sababu ya kuchagua kufikiri vizuri ili kuwa na taifa lenye maendeleo.

Hivyo basi jiongezee maarifa kwa kusoma kitabu hiki na hakika utakombolewa kifikra. Mfalme Sulemani alisema, “Akili ya mtu mwelevu hutafuta maarifa na sikio la mtu mwenye busara hutafuta kusikia maarifa.”

Mwandishi wa kitabu hichi Bw. Denis Mpagaze anaeleza kuwa mafanikio huanza kwanza kwenye fikra za mtu kabla ya kuonekana kwenye matendo. Kitabu hiki kinahamasisha kuondoa hofu, kujiamini, kuwa na maono makubwa, na kutumia uwezo wako wa ndani kwa maendeleo yako.

Pia kinagusia umuhimu wa nidhamu, maamuzi sahihi, mazingira mazuri, pamoja na kujifunza kila siku kama njia ya kujijenga kiakili na kiuchumi. Lugha iliyotumika ni rahisi kueleweka na yenye mifano inayoweza kumgusa msomaji wa kawaida.

Baadhi ya mada zinazopatikana ndani ya kitabu hiki ni Nguvu ya Fikra, Jinsi mawazo yanavyoathiri maisha na mafanikio ya mtu, Umuhimu wa kuamini uwezo wako binafsi, Maono na Malengo ya Maisha

 

Duka
Bei
Angalia
Sh 5,000
Bidhaa
Tafuta
Huduma